Vipimo
Unga 1 ½ Vikombe
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Chumvi ½ Kijiko cha chai
Siagi isiyo na chumvi ½ Kikombe
Sukari 1 Kikombe
Mayai 3
Vanilla 1½ Vijiko vya chai
Maziwa ¾ Kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Washa oveni moto wa 350°. Kisha weka karatasi za kupikia keki za vikombe kwenye treya.
- Katika bakuli la kiasi, chunga pamoja unga, baking powder na chumvi na iache kando.
- Katika bakuli la mashine changanya siagi na sukari hadi ilainike.
- Halafu tia yai moja baada la jengine huku unaendelea kuchanganya, kisha tia vanilla.
- Kisha tia mchanganyiko wa unga uliyoweka kando nusu yake huku unaendelea kuchanganya, kisha tia maziwa na umalizie na unga uliyobakia.
- kisha mimina kwenye treya/karatasi za kuchomea keki za vikombe lakini usijaze mpaka juu.
- Weka katika oveni kwa muda wa dakika 20.
- Ziache zipoe kisha zipake icing/cream upendayo na zitakuwa tayari kuliwa.
Kidokezo
Kipimo hichi ni ya vikeki darzeni moja.
0 comments:
Post a Comment