Follow this blog with bloglovin

Ads

24-Wanyama Na Alivyoumba Allaah Vinathibitisha Tawhiyd

Hud-hud (ndege) alikuwa miongoni mwa jeshi la Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis-Salaam). Aliporuka na kufikia mji wa Sabaa alikuta watu huko wanaabudu jua, akarudi kumpa taarifa Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis-Salaam) kwa kuikansuha ‘ibaadah hiyo batili. Uzuri ulioje ndege huyo kuthibitisha Tawhiyd ya  Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)! Kisa chake kinaanza katika Qur-aan pale alipokosekana katika jeshi la Nabiy Sulaymaan (‘Alayhis-Salaam):
ูˆَุชَูَู‚َّุฏَ ุงู„ุทَّูŠْุฑَ ูَู‚َุงู„َ ู…َุง ู„ِูŠَ ู„َุง ุฃَุฑَู‰ ุงู„ْู‡ُุฏْู‡ُุฏَ ุฃَู…ْ ูƒَุงู†َ ู…ِู†َ ุงู„ْุบَุงุฆِุจِูŠู†َ ﴿ูขู ﴾ ู„َุฃُุนَุฐِّุจَู†َّู‡ُ ุนَุฐَุงุจًุง ุดَุฏِูŠุฏًุง ุฃَูˆْ ู„َุฃَุฐْุจَุญَู†َّู‡ُ ุฃَูˆْ ู„َูŠَุฃْุชِูŠَู†ِّูŠ ุจِุณُู„ْุทَุงู†ٍ ู…ُّุจِูŠู†ٍ ﴿ูขูก﴾ ูَู…َูƒَุซَ ุบَูŠْุฑَ ุจَุนِูŠุฏٍ ูَู‚َุงู„َ ุฃَุญَุทุชُ ุจِู…َุง ู„َู…ْ ุชُุญِุทْ ุจِู‡ِ ูˆَุฌِุฆْุชُูƒَ ู…ِู† ุณَุจَุฅٍ ุจِู†َุจَุฅٍ ูŠَู‚ِูŠู†ٍ ﴿ูขูข﴾ ุฅِู†ِّูŠ ูˆَุฌَุฏุชُّ ุงู…ْุฑَุฃَุฉً ุชَู…ْู„ِูƒُู‡ُู…ْ ูˆَุฃُูˆุชِูŠَุชْ ู…ِู† ูƒُู„ِّ ุดَูŠْุกٍ ูˆَู„َู‡َุง ุนَุฑْุดٌ ุนَุธِูŠู…ٌ ﴿ูขูฃ﴾ ูˆَุฌَุฏุชُّู‡َุง ูˆَู‚َูˆْู…َู‡َุง ูŠَุณْุฌُุฏُูˆู†َ ู„ِู„ุดَّู…ْุณِ ู…ِู† ุฏُูˆู†ِ ุงู„ู„َّู€ู‡ِ ูˆَุฒَูŠَّู†َ ู„َู‡ُู…ُ ุงู„ุดَّูŠْุทَุงู†ُ ุฃَุนْู…َุงู„َู‡ُู…ْ ูَุตَุฏَّู‡ُู…ْ ุนَู†ِ ุงู„ุณَّุจِูŠู„ِ ูَู‡ُู…ْ ู„َุง ูŠَู‡ْุชَุฏُูˆู†َ ﴿ูขูค﴾ ุฃَู„َّุง ูŠَุณْุฌُุฏُูˆุง ู„ِู„َّู€ู‡ِ ุงู„َّุฐِูŠ ูŠُุฎْุฑِุฌُ ุงู„ْุฎَุจْุกَ ูِูŠ ุงู„ุณَّู…َุงูˆَุงุชِ ูˆَุงู„ْุฃَุฑْุถِ ูˆَูŠَุนْู„َู…ُ ู…َุง ุชُุฎْูُูˆู†َ ูˆَู…َุง ุชُุนْู„ِู†ُูˆู†َ ﴿ูขูฅ﴾ ุงู„ู„َّู€ู‡ُ ู„َุง ุฅِู„َู€ٰู‡َ ุฅِู„َّุง ู‡ُูˆَ ุฑَุจُّ ุงู„ْุนَุฑْุดِ ุงู„ْุนَุธِูŠู…ِ ۩﴿ูขูฆ﴾
(Sulaymaan) Akakagua ndege, akasema: “Imekuwaje, mbona simuoni Al-Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walioghibu? Bila shaka nitamuadhibu adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja bayana (ya kughibu kwake).” Basi hakukaa sana (mara alitokeza) akasema: “Nimegundua usilogundua na nimekujia kutoka Sabaa na habari za yakini. Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawamiliki, na amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa. Nimemkuta (yeye) na watu wake wanalisujudia jua badala ya Allaah, na shaytwaan amewapambia ‘amali yao (hiyo), basi akawazuia na njia (ya haki); kwa hiyo hawakuongoka. Hawamsujudii Allaah Ambaye Anatoa yenye kufichika katika mbingu na ardhi na Anayajua yale mnayoyaficha na yale mnayoyadhihirisha. Allaah - hakuna ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, Rabb (Mola) wa Al-‘Arsh adhimu. [An-Naml: 20-26]

Tumepata mafunzo yafuatayo kutokana na ndege huyo Al-Hud-hud:
1.   Alikuwa mwenye ‘Aqiydah swahiyh.
2.   Aikuwa ni mwenye kumwamini Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).
3.   Alikuwa mwerevu kuweza kuchungua na kutambua wanayoyaabudu watu katika safari yake hiyo ya haraka kabisa.
4.   Aliungulika moyoni kuona watu wanakanusha Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Taa’alaa).
5.   Amefanya kazi ya Rasuli kulingania katika Dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).
6.   Jambo kuu alolingania ni la kukanusha shirki na kuthibitisha Tawhiyd.
7.   Ameonya kuhusu udanganyifu, uchochezi wa shaytwaan kuwa anawapambia watu ‘amali zao.
8.   Ametafakari Utukufu wa Muumba wake, neema Zake na uwezo Wake wa kuyajua yaliyo dhahiri na yaliyofichika.
9.   Amefadhilisha Aakhirah kuliko dunia kwani hakujali mali na starehe alizojaaliwa nazo Malkia wa Sabaa.    
10.                 Akathibitisha tena baada yote hayo Tawhiyd ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).

Je, ingekuwaje kama Hud-hud angepitia watu katika zama zetu wanaomshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aa’aa) kwa kila aina ya shirki?  Kisha tujiulize; Je, ni wangapi wenye mfano wa Hud-hud?  Ni dhahiri kwamba Hud-hud alikuwa mbora kuliko baadhi yetu juu ya kuwa yeye ni mnyama dhaifu anayeruka angani. Bali hakikawanyama  na vitu vyote Alivyoumba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) vinashuhudia Tawhiyd kwani vyote vinamsujudia na kumsabbih Allaah (Subhanaahu wa Ta’aalaa) kama Anavyosema:
ุฃَูˆَู„َู…ْ ูŠَุฑَูˆْุง ุฅِู„َู‰ٰ ู…َุง ุฎَู„َู‚َ ุงู„ู„َّู€ู‡ُ ู…ِู† ุดَูŠْุกٍ ูŠَุชَูَูŠَّุฃُ ุธِู„َุงู„ُู‡ُ ุนَู†ِ ุงู„ْูŠَู…ِูŠู†ِ ูˆَุงู„ุดَّู…َุงุฆِู„ِ ุณُุฌَّุฏًุง ู„ِّู„َّู€ู‡ِ ูˆَู‡ُู…ْ ุฏَุงุฎِุฑُูˆู†َ﴿ูคูจ﴾ ูˆَู„ِู„َّู€ู‡ِ ูŠَุณْุฌُุฏُ ู…َุง ูِูŠ ุงู„ุณَّู…َุงูˆَุงุชِ ูˆَู…َุง ูِูŠ ุงู„ْุฃَุฑْุถِ ู…ِู† ุฏَุงุจَّุฉٍ ูˆَุงู„ْู…َู„َุงุฆِูƒَุฉُ ูˆَู‡ُู…ْ ู„َุง ูŠَุณْุชَูƒْุจِุฑُูˆู†َ﴿ูคูฉ﴾ ูŠَุฎَุงูُูˆู†َ ุฑَุจَّู‡ُู… ู…ِّู† ูَูˆْู‚ِู‡ِู…ْ ูˆَูŠَูْุนَู„ُูˆู†َ ู…َุง ูŠُุคْู…َุฑُูˆู†َ ۩﴿ูฅู ﴾
Je, hawaoni vile vitu Alivyoumba Allaah ambavyo vivuli vyake vinaelemea kulia na kushoto vikimsujudia Allaah na huku vinanyenyekea? Na ni kwa Allaah pekee vinasujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo na Malaika, nao hawatakabari. Wanamkhofu Rabb (Mola) wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa. [An-Nahl: 48-50]

Na Anasema pia:

ุฃَู„َู…ْ ุชَุฑَ ุฃَู†َّ ุงู„ู„َّู€ู‡َ ูŠَุณْุฌُุฏُ ู„َู‡ُ ู…َู† ูِูŠ ุงู„ุณَّู…َุงูˆَุงุชِ ูˆَู…َู† ูِูŠ ุงู„ْุฃَุฑْุถِ ูˆَุงู„ุดَّู…ْุณُ ูˆَุงู„ْู‚َู…َุฑُ ูˆَุงู„ู†ُّุฌُูˆู…ُ ูˆَุงู„ْุฌِุจَุงู„ُ ูˆَุงู„ุดَّุฌَุฑُ ูˆَุงู„ุฏَّูˆَุงุจُّ ูˆَูƒَุซِูŠุฑٌ ู…ِّู†َ ุงู„ู†َّุงุณِ ۖ ูˆَูƒَุซِูŠุฑٌ ุญَู‚َّ ุนَู„َูŠْู‡ِ ุงู„ْุนَุฐَุงุจُ ۗ ูˆَู…َู† ูŠُู‡ِู†ِ ุงู„ู„َّู€ู‡ُ ูَู…َุง ู„َู‡ُ ู…ِู† ู…ُّูƒْุฑِู…ٍ ۚ ุฅِู†َّ ุงู„ู„َّู€ู‡َ ูŠَูْุนَู„ُ ู…َุง ูŠَุดَุงุกُ ۩﴿ูกูจ﴾
Je, huoni kwamba Allaah wanamsujudia walioko mbinguni na ardhini, (na vinamsujudia pia) jua, na mwezi na nyota, na majabali na miti na viumbe vinavyotembea, na wengi miongoni mwa watu? Na wengi (miongoni mwa watu pia) imewathibitikia adhabu. Na ambaye Allaah Amemdhalilisha, basi hatopata wa kumkirimu. Hakika Allaah Anafanya Atakavyo.  [Al-Hajj: 18]

Na pia:
ุชُุณَุจِّุญُ ู„َู‡ُ ุงู„ุณَّู…َุงูˆَุงุชُ ุงู„ุณَّุจْุนُ ูˆَุงู„ْุฃَุฑْุถُ ูˆَู…َู† ูِูŠู‡ِู†َّ ۚ ูˆَุฅِู† ู…ِّู† ุดَูŠْุกٍ ุฅِู„َّุง ูŠُุณَุจِّุญُ ุจِุญَู…ْุฏِู‡ِ ูˆَู„َู€ٰูƒِู† ู„َّุง ุชَูْู‚َู‡ُูˆู†َ ุชَุณْุจِูŠุญَู‡ُู…ْ ۗ ุฅِู†َّู‡ُ ูƒَุงู†َ ุญَู„ِูŠู…ًุง ุบَูُูˆุฑًุง ﴿ูคูค﴾
Zinamsabbih mbingu saba na ardhi na vilivyomo humo. Na hakuna kitu chochote isipokuwa kinasabbih kwa Sifa Zake njema, lakini hamzifahamu tasbiyh zao. Hakika Yeye daima ni Haliyman-Ghafuwraa (Mpole wa kuvumilia waja - Mwingi wa kughufuria). [Al-Israa: 44]
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: