Follow this blog with bloglovin

Ads

MAANDAZI / MAHAMRI (English and Swahili )


Unga wa ngano nusu kilo
Hamira kijiko 1 cha supu 
Sukari vijiko 3 mpaka 5 vya supu 
Iliki iliyosagwa kijiko 1 cha supu 
Nazi (tui zito)  vijiko 5 vya supu 
Mafuta ya kula lita 1 (kwa ajili ya kuchomea)   
Maji ya uvugu vugu( ya kukandia  ) Kwenye bakuli tia maji ya uvugu vugu nusu kikombe ,tia hamira funika kwa dakika 3  hadi 5, kisha tia sukari koroga vizuri na uanze kutia unga wa ngano na iliki kidogo kidogo  huku unachanganya
 Tia tui ,anza kukanda unga engeza maji yakihitajika mpaka donge lishikane vizuri ,kanda kwa dakika 15 mpaka 20 au mpaka  liwe laini na  halinati kwenye vidole vyako. Ugawe madonge 3 au 4 sawa sawa yafanye duara 
Sehem utakayokatia mandazi weka/nyunyiza unga kidogo chukua donge moja moja lisukume kutumia kifimbo cha chapati lakini lisiwe jembamba sana wala nene sana , kulingana na ukubwa unaopenda Tumia kisu  kata mara 2 kupata pisi 4        
PIC NO 1.
Ukimaliza yote yaweke pembeni sehem yenye joto yaumuke / yafure  mara mbili yake Teleka mafuta kwenye karai yakipata moto tia maandazi ,yakiwiva upande mmoja geuza upande wa pili mpaka yaiwive na yapige rangi ya brown  yatoe ,yapo tayari kuliwa kwa chai au mchuzi.
  
PIC NO 2.
       
PIC NO 3    
ENGLISH
 Plain flour half kg 
Yeast 1 tbsp Sugar 3 to 5 tbsp 
Cardamom powder 1 tbsp 
Coconut cream 5 tbsp 
Cooking oil 1 littre 
Warm water for kneading 
In a bowl put 1/2 of warm water  add yeast ,cover for 3 to 5 mins ,then add sugar mix well together, start  adding flour and  cardamom powder, mix well add coconut milk and more water if required, knead for 15 to 20 mins or until smooth and it doesn’t stick to your fingers 
Divide in to 3 to 4 small doughs  (equal size)and make them a perfect round 
Dust a flour on your work surface,using a rolling pin ,roll each round to make a good size depend on the size you want ,use a knife to cut  in to 4 quarters  ( see pic no 1) let them rise 
In a pan heat the oil on a medium heat,  when the oil is hot add your mandazi and start fryng one side until done flip the other side  until golden brown remove them ,serve with tea or curry.
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: