Follow this blog with bloglovin

Ads

11-Neno La Tawhiyd Ni Miongoni Mwa Maneno Ayapendao Allaah Na Rasuli

Kutoka kwa Samurah bin Jundub (Radhwiya-Allaahu ‘anhu) ambaye amesema:

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((أَحًبُّ الْكَلامِ إِلَى اللَّهِ أَرْبَعٌ: سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلا إِلَهَ إِلا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، لا يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأْتَ))
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Bora ya maneno kwa Allaah ni manne: Subhaana-Allaah, walhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar, wa laa hawla wa laa quwwata illaa biLLaah - Utakasifu ni wa Allaah na Sifa njema ni za Allaah, na  hapana muabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa.… si vibaya kuanza kwa lolote katika hayo))  [Muslim]

Na Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu):

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((لأَنْ أَقُولَ: سُبْحَانَ اللهِ، والحَمْدُ للهِ، وَ لاَ إَلَهَ إلاَّ اللهُ، واللهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إَلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ))
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Kusema kwangu:Subhaana-Allaah, WalhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar- Utakasifu ni wa Allaah na Sifa njema ni za Allaah, na hapana muabudiwa wa haki  ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa.… ni bora kwangu kuliko kila kilichoangaziwa na jua))   [Muslim]

Na Hadiyth ya ya Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu):

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((إِنَّ أَفْضَلَ الدُّعَاءِ: الْحَمْدُ لِلَّه، وَأَفْضَلُ الذِّكْرِ: لاَ إلَهَ إِلاَّ الله))
Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: ((Bora ya du’aa ni mtu kusema: AlhamduliLlaah- Sifa njema  ni za Allaah, na dhikri bora ni: laa ilaaha illa-Allaah - Hapana muabudiwa wa haki ila Allaah)) [At-Tirmidhiy, ibn Maajah. Al-Haakim na ameisahihisha na ameiwafiki Adh-Dhahaby na angalia: Swahiyh Al-Jaami (1/362) [1104]

Na maneno hayo yana thawabu nzito, mbele ya Allah na ndiyo ’amali zinazotangulia na kubakia Aakhirah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa):
الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا ﴿٤٦﴾
Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. Na Al-Baaqiyaatu Asw-Swaalihaatu (‘amali nzuri zibakiazo) ni bora mbele ya Rabb (Mola) wako, kwa thawabu na matumaini.  [Al-Kahf: 46]
Akataja Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuhusu Aayah hiyo kuwa miongoni mwa 'amali zilokusudiwa ni kusema pia: “Subhaana Allaah, wal-HamduliLlaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar [Tafsiyr Ibn Kathiyr]
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: