Follow this blog with bloglovin

Ads

10-Tawhiyd Ni Haki Yake Allaah (Subhaanahu Wa Ta'alaa)

Ameamrisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kuabudiwa bila ya kumshirikisha na kitu au kumlinganisha na yeyote au chochote kile: 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿٢١﴾ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾
Enyi watu! Mwabuduni Rabb (Mola) wenu Ambaye Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimuwekee Allaah waliolingana naye (washirika) na hali ya kuwa nyinyi mnajua (kuwa hakuna kinacholingana Naye). [Al-Baqarah: 21-22]

Na Anaamrisha pia:
 وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ
Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. [An-Nisaa: 36]

 وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ
Na Rabb (Mola) wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu (yeyote) isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili [Al-Israa: 23]

 وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ
Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (awaamrishe watu wake) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuwt (miungu ya uongo). [An-Nahl: 36]
Na katika miongoni mwa wasiyyah kumi wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kwa Rasuli Wake:
قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ
Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb (Mola) wenu kwenu. (Anaamrisha) Kwamba msimshirikishe na chochote. [Al-An’aam: 151]
Na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akausia kwa Swahaba zake:
عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: كُنْتُ رَدِيفَ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) عَلَى حِمَارٍ فَقَالَ لِي: ((يَا مُعَاذُ؟ أَتَدْرِي مَا حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ, وَمَا حَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ؟)) قُلْتُ اَللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ, قَالَ: ((حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ أَنْيَعْبُدُوهُ, وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا, وَحَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ أَنْ لاَ يُعَذِّبَ مَنْ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا)) قُلْتُ يَارَسُولَ اَللَّهِ أَفَلاَ أُبَشِّرُ اَلنَّاسَ؟ قَالَ: ((لاَ تُبَشِّرْهُمْ فَيَتَّكِلُوا)) أَخْرَجَاهُ فِي اَلصَّحِيحَيْنِ
Imepokelewa toka kwa Mu’aadh bin Jabal(رضي الله عنه)  amesema: Nilikuwa nyuma ya Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) nimepanda punda akasema: ((Ee Mu’aadh! Unajua nini haki ya Allaah juu wa waja Wake na haki ya waja juu ya Allaah?)) Nikajibu: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi: Akasema: ((Haki ya Allaah kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote. Na haki ya waja kwa Allaah ni kwamba Hatomwadhibu yeyote ambaye hamshirikishi na kitu)). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Nibashirie watu? Akasema: ((Usiwabashirie wasije kuitegemea)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: