Follow this blog with bloglovin

Ads

09-Aina Zote Tatu za Tawhiyd Zinaafikiana, Haiwezekani Kukosekana mojawapo

Aina zote Tatu za Tawhiyd zinaafikiana. Kutokuamini mojawapo humtoa mtu nje ya Uislamu kwa sababu makafiri Quraysh waliamini Tawhiydur-Rubuwbiyyah wakakanusha ya Uluwhiyyah. Waliamini kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Ndiye Muumba wao, na Ndiye Muumba wa mbingu na ardhi, Ndiye Anayendesha mambo yote, Ndiye Anayewaruzku, Na Ndiye Anayeteremsha mvua n.k. Dalili kadhaa katika Qur-aan:

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٨٧﴾
Na ukiwauliza: Ni nani kawaumba? Bila shaka watasema: “Allaah.”  Basi vipi mnaghilibiwa (kumshirikisha Allaah)? [Az-Zukhruf: 87]

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٥﴾
Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” bila shaka watasema: “Allaah.” Sema: “AlhamduliLLaah (Sifa njema zote ni za Allaah).” Bali wengi wao hawajui. [Luqmaan: 25]

 وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّـهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ ۚ قُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ ۖ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ ﴿٣٨﴾
Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah; ikiwa Allaah Atanitakia dhara; je, wao wataweza kuondosha dhara Yake? Au Akinitakia Rahmah; je wao wataweza kuizuia Rahmah Yake?” Sema: “Ananitosheleza Allaah”, Kwake watawakali wenye kutawakali.  [Az-Zumar: 38]

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٦١﴾ اللَّـهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٦٢﴾ وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ مَوْتِهَا لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٦٣﴾
Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi, na akatiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Basi wapi wanaghilibiwa (kutokumwamini Allaah)?  Allaah Humkunjulia riziki Amtakaye katika waja Wake na Humdhikishia (Amtakaye). Hakika Allaah kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi). Na ukiwauliza: “Ni nani Ateremshaye maji (mvua) kutoka mbinguni, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake?” Bila shaka watasema: “Allaah”.  Sema: “AlhamduliLLaah (Sifa njema zote ni za Allaah).” Bali wengi wao hawatii akilini. [Al-‘Ankabuwt: 61 -63]

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٣١﴾
Sema: (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini. Au nani anayemiliki kusikia na kuona; na nani anayemtoa (aliye) hai kutoka mfu, na anayemtoa mfu kutoka (aliye) uhai; na nani anayedabiri mambo (yote)?   Watasema: “Ni Allaah”; basi sema: “Je basi hamuwi na taqwa?” (kumkhofu Allaah?) [Yuwnus: 31]
Lakini walimshirikisha katika ‘ibaadah zao wakidai kuwa walivyokuwa wakiviabudu vinawakaribisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa):
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ ﴿٣﴾
Na wale waliojichukulia badala Yake awliyaa (walinzi, wasaidizi) (wakisema): “Hatuwaabudu isipokuwa kwa (lengo la) kutukurubisha kwa Allaah ukaribu.” Hakika Allaah Atahukumu baina yao katika yale (yote) waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah Hamuongozi aliye muongo, kafiri) [Az-Zumar: 3]

Qur-aan ikathibitisha tena na tena kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Ndiye wa kuabudiwa katika Rubuwbiyyah (Uola, Umiliki, Uendeshaji wa Ulimwengu, Uumbaji, Utoaji rizki, Uhuishaji na Ufishaji, n.k.) Yake na Uluwhiyyah (‘ibaadah) Yake, 

اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٤﴾ هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۗ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٦٥﴾
Allaah Ambaye Amekujaalieni ardhi kuwa mahali pa makazi, na mbingu kama ni paa na Akakusawirini, Akazifanya nzuri zaidi sura zenu, na Akakuruzukuni katika vizuri. Huyo Ndiye Allaah Rabb (Mola) wenu. Basi Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu. Yeye Ndiye Al-Hayyu (Aliye Hai daima), hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye; basi muombeni Yeye mukhliswiyn (wenye kumtakasia) Dini. AlhamduliLLaahi (Sifa njema zote ni za Allaah) Rabb (Mola) wa walimwengu. [Ghaafir: 64- 65]

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١﴾ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾
Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana waladi na hali hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye kwa kila kitu ni ‘Aliym (Mjuzi). Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb (Mola) wenu. Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Wakiyl Mtegemewa wa kuendesha mambo). [Al-An’aam: 101-102]
ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٦٢﴾
Huyo Ndiye Allaah Rabb (Mola) wenu, Khaaliq (Muumba) wa kila kitu, hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye; basi vipi mnaghilibiwa (kumshirikisha)? [Ghaafir: 62]

 خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ يُكَوِّرُ اللَّيْلَ عَلَى النَّهَارِ وَيُكَوِّرُ النَّهَارَ عَلَى اللَّيْلِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ أَلَا هُوَ الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ ﴿٥﴾ خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٦﴾
Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki, Anaufunika usiku juu ya mchana, na Anafunika mchana juu ya usiku, na Anatiisha jua na mwezi; kila kimoja kinakwenda mpaka muda maalumu uliopangwa. Tanabahi! Yeye Ndiye Al-‘Aziyzul-Ghaffaar (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima Mwingi wa kughufuria). Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, kisha Akajaalia humo mwenziwe (mke), na Akakuteremshieni katika wanyama wa mifugo jozi nane (madume na majike; ngamia, ng’ombe, kondoo na mbuzi). Anakuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyo Ndiye Rabb (Mola) wenu Pekee Ana ufalme, Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, basi vipi mnageuzwa (akili yenu inakupelekeni kumwabudu asiyekuwa Allaah?).  [Az-Zmuar 5 – 6]

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ هَلْ مِنْ خَالِقٍ غَيْرُ اللَّـهِ يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٣﴾
Enyi watu! Kumbukeni neema za Allaah kwenu. Je, kuna muumbaji yeyote (yule) badala ya Allaah Anayekuruzukuni kutoka mbinguni na (kwenye) ardhi? Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, basi kutoka wapi mnaghilibiwa (kumshirikisha)?.[Faatwir: 3]

 أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ ﴿١١٥﴾ فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ﴿١١٦﴾ وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿١١٧﴾
“Je, mlidhania kwamba Sisi Tulikuumbeni bila kusudio (kwa burudani na mchezo tu?); na kwamba nyinyi Kwetu hamtorejeshwa?” Basi Ta’ala-Allaah (Ametukuka Allaah) Al-Malikul-Haqqu (Mfalme wa haki). Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. Rabb (Mola) wa Al-‘Arsh tukufu.  Na yeyote yule anayeomba (Du’aa au kuabudu) pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Rabb (Mola) wake. Hakika hawafaulu makafiri.   [Al-Muuminuwn: 115-117]

رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ ﴿٧﴾  لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ ﴿٨﴾
Rabb (Mola) wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, mkiwa ni wenye yakini. Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, Anahuisha na Anafisha; Rabb (Mola) wenu na Rabb wa baba zenu wa awali.  [Ad-Dukhaan: 7- 8]

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴿٣﴾
Hakika Rabb (Mola) wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah). Anadabiri mambo (ya kila Alichokiumba). Hakuna mwombezi yeyote ila baada ya idhini Yake. Huyu Ndiye Allaah Rabb Wenu, basi mwabuduni. Je, hamkumbuki? [Yuwnus: 3]

Anathibitisha pia kuhusu Tawhiyd Yake ya Asmaa na Swifaat kwamba inaafikiana na Tawhiyd ya Rubuwbiyyah na Uluwhiyyah.
 اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ﴿٨﴾
Allaah, hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye ila Yeye. Anayo Majina Mazuri kabisa [Twaahaa: 8]
وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾
Na Ilaah wenu (Muabudiwa wa haki) ni Ilaahun-Waahid (Muabudiwa wa haki Mmmoja tu) hapana ilaaha ila Yeye. (Ar-Rahmaanur-Rahiym (Mwingi wa Rahmah - Mwenye kurehemu).” [Al-Baqarah: 163]
إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦٢﴾
Hakika haya ni masimulizi ya haki. Na hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) isipokuwa Allaah. Na hakika Allaah Yeye Ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvuAsiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima).  [Aal-‘Imraan: 62]

Kuwa na ujuzi kuhusiana na Tawhiyd ya Asmaa wasw-Swifaat (Majina na Sifa za Allaah) utamtambua Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) vizuri kabisa na hutokuwa mwenye kukanusha, na itakuepusha na kupotoa maana ya Majina na Swiffah Zake na kuzibadilisha maana au kumfananisha na viumbe vyenginevyo
قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ
Sema; “Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah). Vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. [Al-Israa: 110]

الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا ﴿٥٩﴾ وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اسْجُدُوا لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا وَمَا الرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ۩ ﴿٦٠﴾
Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah), Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah), basi ulizia habari Zake. Na wanapoambiwa: “Msujudieni Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah)” husema: “Ni nani huyo Ar-Rahmaan? Tumsujudie unayetuamrisha, na inawazidishia kukengeuka. [Al-Furqaan: 59 – 60]

كَذَٰلِكَ أَرْسَلْنَاكَ فِي أُمَّةٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهَا أُمَمٌ لِّتَتْلُوَ عَلَيْهِمُ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَـٰنِ ۚ قُلْ هُوَ رَبِّي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ مَتَابِ ﴿٣٠﴾
Hivyo ndivyo Tumekutuma katika Ummah uliokwishapita kabla yake umati nyingine ili uwasomee yale Tuliyokufunulia Wahy; nao wanamkanusha Ar-Rahmaan. Sema: “Yeye Ndiye Rabb (Mola) wangu; Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. Kwake natawakali na Kwake ni marejeo yangu.” [Ar-Ra’d: 30]
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: