Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Anasema:
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ﴿٥٦﴾
Na Sikuumba majini na wanaadamu isipokuwa waniabudu [Adh-Dhaariyaat: 56]
Anatujulisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kwamba Ametuumba kwa hikmah nayo ni kumpwekesha katika ‘ibaadah wala hakutuumba kwa kuwa Ana haja nasi kwani yeye ni Al-Ghaniyy (Mkwasi Asiyehitaji kitu) kama Anavyosema:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ﴿١٥﴾
Enyi watu! Nyinyi ni mafakiri kwa Allaah! Na Allaah Ndiye Al-Ghaniyyul-Hamiyd (Mkwasi - Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote daima). [Faatwir: 15]
Akathibitisha hayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Anapoendelea kusema:
مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ﴿٥٧﴾
Sitaki kutoka kwao riziki yoyote, na wala (Sitaki) wanilishe. [Adh-Dhaariyaat: 57]
Akatujulisha kwamba Hahitaji lolote kutoka kwa waja Wake, bali waja ndio wanaomhitaji Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kwani Yeye Ndiye Anayewaruzuku na Anawaendeshea maisha yao na Ndiye Anayewapangia na kuwatengeneza mambo yao. Yeye ni Allaah, Anayestahiki kuabudiwa kwa haki Naye Ndiye Muumba wa kila kitu:
ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ﴿١٠٢﴾
Huyo kwenu Ndiye Allaah, Mola wenu. Hapana ilaaha (mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Wakiyl (Mtegemewa kwa yote). [Al-An’aam: 102]
Na Anasema pia:
ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٦٢﴾
Huyo Ndiye Allaah Mola wenu, Khaaliq (Muumba) wa kila kitu, hapana ilaaha (mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ila Yeye; basi vipi mnageuzwa? [Ghaafir: 62]
Viumbe hao, wanajumuika Malaika, majini na wanaadamu. Wote hao wanastahiki kumwambudu kwa kuwa ni haki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kutoka kwao na lau kama watamshirikisha, basi Atawaadhibu hata ikiwa Malaika watamshirikisha, kama Anavyosema:
وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ
Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema (kuwa): “Mimi ni ilaahu (mungu) pasi Naye,” basi huyo Tutamlipa (Moto wa) Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu. [Al-Anbiyaa: 29]
Na atakayemshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) hatoweza kufidia kuepuka na adhabu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) hata akiwa na dhahabu inayojaa ardhini! Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa):
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾
Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitokubaliwa kutoka kwa mmoja wao (fidia ya) dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wakitaka kujikombolea nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru.[Aal-‘Imraan: 91]
0 comments:
Post a Comment