Follow this blog with bloglovin

Ads

12-Vitabu Vya Mbinguni Vimeteremshwa Kuamrisha Tawhiyd

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ الْبَيِّنَةُ﴿١﴾رَسُولٌ مِّنَ اللَّـهِ يَتْلُو صُحُفًا مُّطَهَّرَةً﴿٢﴾فِيهَا كُتُبٌ قَيِّمَةٌ﴿٣﴾وَمَا تَفَرَّقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَتْهُمُ الْبَيِّنَةُ﴿٤﴾وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚوَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ﴿٥﴾
Hawakuwa wale waliokufuru miongoni mwa ahlil-Kitaabi (Mayahudi na Manaswara) na washirikina wenye kuacha (waliyonayo) mpaka iwafikie hoja bayana.
Rasuli kutoka kwa Allaah anawasomea sahifa zilotwaharika.
Ndani yake humo mna maandiko yanayosimama imara.
Na hawakufarikiana wale waliopewa kitabu isipokuwa baada ya kuwajia hoja bayana.
Na hawakuamrishwa (chochote kile) isipokuwa wamwabudu Allaah mukhliswiyn (wenye kumtakasia) Dini, hunafaa(wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki) na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara.
[Al-Bayyinah: 1- 5]

Na Anasema pia:
إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚوَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾
Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Nabiy baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw (vizazi) na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, Na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwraa.
[An-Nisaa: 163]

Na Anasema:

 الم﴿١﴾ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ﴿٢﴾ نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ﴿٣﴾ مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗإِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤﴾
Alif Laam Miym.
Allaah, hakuna ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, Al-Hayyul-Qayyuwm (Aliyehai daima - Msimamia kila kitu).
Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na Akateremsha Tawraat na Injiyl.
Kabla, ni mwongozo kwa watu na Akateremsha al-furqaan. Hakika wale waliokanusha Aayaat za Allaah watapata adhabu kali. Na Allaah ni ‘Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima) Mwenye kulipiza.
[Aal-‘Imraan: 1-4]

Na Anasema Subhaanahu wa Ta’aalaa:

الر ۚ كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ﴿١﴾ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ﴿٢﴾
Alif Laam Raa. Kitabu ambacho Aayaat Zake zimetimizwa barabara, kisha zikafasiliwa (vyema) kutoka kwaHakiymin-Khabiyr (Mwenye hikmah wa yote daima - Mjuzi wa vilivyodhahiri na vilivyofichikana).
(Kupitia kwa Rasuli ili) “Usiabudu isipokuwa Allaah”. “Hakika mimi ni mwonyaji kwenu na mbashiriaji.”
 [Huwd: 1-2]

Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kutokana na Hadiyth ya Abu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

الْأَنْبِيَاءُ إِخْوَةٌ مِنْ عَلَّاتٍ، وَأُمَّهَاتُهُمْ شَتَّى، وَدِينُهُمْ وَاحِد))
((Manabii ni ndugu kwa baba na mama zao ni mbalimbali, na Dini yao ni moja)) [Muslim]

Wanasema Wanachuoni kutokana na Hadiyth hii kuwa, Manabii wote asli ya Iymaan yao ni moja, na Shari’ah zao ni tofauti, lakini wote wanaungana na kuafikiana wote kwa Tawhiyd yao ambayo ni moja.
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: