Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Anasema:
وَهُوَ اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْحَمْدُ فِي الْأُولَىٰ وَالْآخِرَةِ ۖ وَلَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٧٠﴾
Naye ni Allaah, Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. Ni Zake Pekee Sifa njema zote za mwanzoni (duniani) na za Aakhirah. Na Hukumu ni Yake Pekee, na Kwake Pekee mtarejeshwa. [Al-Qaswasw: 70]
Mwanzoni kabla ya uhai:
هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾
Yeye Ndiye Aliyekutieni sura katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima). [Aal-‘Imraan: 6]
خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٦﴾
Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, kisha Akamfanya humo mwenziwe (mke), na Akakuteremshieni katika wanyama wa mifugo jozi nane (madume na majike; ngamia, ng’ombe, kondoo na mbuzi). Anakuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyo Ndiye Rabb(Mola) wenu Pekee Ana ufalme, Hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye, basi vipi mnageuzwa (kumwabudu asiyekuwa Allaah?).[Az-Zumar: 6]
Mwishoni:
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۗ وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ حَدِيثًا﴿٨٧﴾
Allaahu hapana ilaaha (muabudiwa wa) ila Yeye. Kwa yakini, Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah haina shaka ndani yake. Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?[An-Nisaa: 87]
0 comments:
Post a Comment