Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Amethibitisha Tawhyd Mwenyewe katika Aayah kadhaa; baadhi yake zifuatazo:
شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾
Allaah Ameshuhudia kwamba hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye; na Malaika, na wenye elimu (wote wameshuhudia kwamba Yeye) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana ilaaha ila Yeye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima). [Aal-‘Imraan: 18]
وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾
“Na Ilaah (Muabudiwa wa haki) wenu ni Ilaahun-Waahid (Muabudiwa wa haki Mmmoja) hapana ilaaha ila Yeye. (Ar-Rahmaanur-Rahiym (Mwingi wa Rahmah - Mwenye kurehemu).” [Al-Baqarah: 163]
Alipompa Nabiy Muwsaa Ujumbe:
إِنَّنِي أَنَا اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ لِذِكْرِي﴿١٤﴾
“Hakika mimi ni Allaah hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Mimi; basi niabudu, na simamisha Swalaah kwa dhikri[1] Yangu.” [Twaahaa: 14]
إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ ﴿٩٢﴾
Hakika huu Ummah wenu ni Ummah mmoja; Nami ni Rabb (Mola) wenu, basi niabuduni. [Al-Anbiyaa: 92]
هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ﴿٢٢﴾هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٢٣﴾هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٢٤﴾
Yeye ni Allaah, Ambaye hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. ‘Aalimu (Mjuzi) wa ghayb na dhahiri, Yeye Ndiye Ar-Rahmaanur-Rahiym (Mwingi wa Rahmah - Mwenye kurehemu). Yeye Ndiye Allaah Ambaye hapana ilaaha (mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ila Yeye, Al-Malik (Mfalme), Al-Qudduws (Mtakatifu), As-Salaam (Mwenye amani), Al-Muumin (Mwenye kusadikisha), Al-Muhaymin (Mwenye kutawala na kuendesha), Al-‘Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima), Al-Jabbaar (Asiyeshindwa kufanya Atakalo), Al-Mutakabbir (Mwenye kustahiki kiburi), Subhaana Allaah! (Utakasifu ni wa Allaah!) kwa yale yote wanayomshirikisha (nayo).Yeye Ndiye Allaah, Al-Khaaliq (Muumbaji), Al-Baariu (Mwanzishi viumbe bila kasoro), Al-Muswawwir (Mtengeneza sura), Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee (kila) kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Al-‘Aziyzul-Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima - Mwenye hikmah wa yote daima). [Al-Hashr: 22-24]
[1]Kumdhukuru Allaah kwa kila aina; kukumbuka Utukufu Wake, neema Zake, ihsani Yake kwa kutaja jina Lake; kumsabbih, kumpwekesha, kumshukuru, kumsifu, kumtukuza, kuomba maghfirah, kusoma Qur-aan, kumswalia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), na kwa kuzingatia na kuyataamali Majina Yake Matukufu.
0 comments:
Post a Comment