Follow this blog with bloglovin

Ads

02-Tawhiyd Inahusiana Na Asmaaul-Husnaa Na Swifaat

Tawhiyd inahusiana na Asmaaul-Husnaa na Swifaat (Majina Mazuri na Sifa za Allaah). Ndio maana Aayatul Kursiyy ikawa ni Aayah bora kabisa katika Qur-aan na Suwratul-Ikhlaasw ikawa ni sawa na thuluthi ya Qur-aan kwa sababu ndani yake zinaelezea Majina na Sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa).

Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Anasema:
اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾
Allaah, hapana ilaaha (mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki) ila Yeye, Al-Hayyul-Qayyuwm (Aliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu). Haumchukuwi usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai (anayeombea) mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawadiriki kitu chochote kile katika Elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Al-‘Aliyyul-‘Adhwiym (Mwenye Uluwa - Mwenye taadhima)[Al-Baqarah: 255]

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾ اللَّـهُ الصَّمَدُ﴿٢﴾  لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾
Sema: “Yeye ni Allaahu Ahad (Mmoja Pekee). Allaah ni Asw-Swamad (Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote). “Hakuzaa na wala Hakuzaliwa. Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana (au kulingana) Naye.”[Ikhlaasw: 112]
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: