Follow this blog with bloglovin

Ads

01-Tawhiyd Ni Elimu Tukufu Na Bora Kabisa

Binaadamu anahitaji kujifunza atambue maana, fadhila na umuhimu wa  Tawhiyd, kisha afanyie kazi kuithibitisha.. 
Elimu ya Tawhiyd ni tukufu na bora kwa kuwa ni elimu anayoihitaji mja kila wakati, kwa sababu inahusiana na Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Ambaye Anapasa kupwekeshwa katika ‘ibaadah bila ya kumshirikisha. Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Anasema:

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ
Basi jua (ee Muhammad صلى الله عليه وسلم) kwamba laa ilaaha illa-Allaah (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Allaah), na omba maghfirah kwa dhambi zako na (kwa dhambi za) Waumini wa kiume na Waumini wa kike. [Muhammad: 19]
Aayah hiyo imetanguliza elimu ya asasi ya Dini nayo ni maarifa ya Tawhiyd, 
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ
Basi jua (ee Muhammad (صلى الله عليه وسلم kwamba laa ilaaha illa-Allaah (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Allaah),

kisha ikafuatia na maarifa ya elimu ya matawi ambayo ni kuomba maghfirah,
وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ
na omba maghfirah kwa dhambi zako na (kwa dhambi za) Waumini wa kiume na Waumini wa kike

Kwa hiyo imethibitisha ubora wa elimu ya Tawhiyd kabla ya ‘amali za mwanaadamu, sababu ‘ibaadah na ‘amali za binaadamu bila ya kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) hazikubaliwi na Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa).
Juu ya kuwa Aayah hiyo imeteremshwa kumkusudia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), lakini haimaanishi kwamba hiyo ni amri kwake kwamba amjue Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa), kwani ujuzi wa kumjua Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) umeshafunuliwa Wahyi kwake kabla ya hapo. Aayah hiyo imeteremshwa akiwa Madiynah na kabla yake imepita miaka 13 akiwa ni Rasuli mjini Makkah akiwalingania watu wake neno hilo la ilaaha illa Allaah. Lilokusudiwa ni kule kutajwa mwanzo elimu ya kumjua Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) kabla ya elimu ya ‘amali kama hivyo kuomba maghfirah, au ‘amali nyinginezo kama Swalaah, Zakaah, Swawm, Hajj na kadhaalika.

Akathibitisha Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu ujuzi wake kuhusiana na Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) akasema:
 فَوَاللَّهِ إنِّي لَأَعْلَمُكُمْ بِاَللَّهِ وَأَشَدُّكُمْ لَهُ خَشْيَة  رواه البخاري
Wa-Allaahi, (Naapa kwa Allaah) kwamba hakika mimi namjua zaidi Allaah na ni mwenye kumkhofu zaidi kuliko nyinyi. [Al-Bukhaariy]

Na ‘amali hazikubaliwi isipokuwa baada ya kumwamini Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Imethibiti kutoka kwa Abu Huraryah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba aliulizwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

أَيُّ الْعَمَلِ أَفْضَلُ؟ فَقَالَ: ((إِيمَانٌ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ))
‘Amali ipi bora kabisa? Akajibu: ((Kumwamini Allaah na Rasuli Wake)). [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) - imehadithiwa na Al-Bukhaariy]
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: