Follow this blog with bloglovin

Ads

03-Tawhiyd Ni Fitwrah (Maumbile Ya Mwanaadam Ya Asili)

Allaah (Subhaanahu wa Ta'alaa) Anasema:

فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Basi elekeza uso wako kwenye Dini ya haniyfaa (kuelemea haki). Fitwrah (maumbile ya mwanaadam ya asili) ya Allaah Aliyowaumbia watu (wote). Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah. Hivyo ndio Dini iliyonyooka sawasawa, lakini watu wengi hawajui. [Ar-Ruwm: 30]

Na Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا مِنْ مَوْلُودٍ إِلَّا يُولَدُ عَلَى الْفِطْرَةِ  فَأَبَوَاهُ يُهَوِّدَانِهِ ، وَيُنَصِّرَانِهِ  وَيُمَجِّسَانِهِ  كَمَا تُنْتَجُ  الْبَهِيمَةُ بَهِيمَةً جَمْعَاءَ ، هَلْ تُحِسُّونَ فِيهَا مِنْ جَدْعَاءَ؟)) ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ: وَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: ((فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ))  
Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba alikuwa akisema: Rasuli  (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  amesema; ((Hakuna kizazi kinachozaliwa (mtoto mchanga) isipokuwa anazaliwa katika 'fitwrah' kisha wazazi wake (humbadilisha na) humuingiza katika dini ya Uyahudi, au Unasara au Umajusi, kama mfano mnyama mwenye pembe anavyomzaa mnyama mwenye pembe kama yeye, je, mtahisi kuwa hana pembe?   Kisha Abu Hurayrah akasema: Someni mkipenda: (kauli ya Allaah):  ((Fitwrah (maumbile ya mwanaadam ya asili) ya Allaah Aliyowaumbia watu (wote). Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah))  [Al-Bukhaariy na Muslim]
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: