Ka'ak ( Keki Kavu Ya Kiarabu)
Vipimo
Unga wa ngano - 3 Vikombe
Unga wa atta - 2 Vikombe
Sukari guru - 1 Kikombe cha chai
Samli au mafuta - 1 Kikombe
Mayai - 4 Makubwa
Sukari nyeupe - 1 Kikombe cha chai
Mdalasini ya unga - 2 Vijiko vya supu
Illiki ya unga - 1 Kijiko cha supu
Habbe soda - 1 Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika bakuli kubwa, changanya pamoja unga wa ngano, unga wa atta, mdalasini, illiki na habbe soda (ukipenda isage).
- Yeyusha sukari guru na samli au mafuta katika moto hadi ichemke kidogo tu.
- Kisha mimina katika mchanganyiko wa unga huku una koroga ichanganyikane vizuri.
- Halafu changanya mayai pamoja na sukari nyeupe katika kibakuli, kisha mimina katika mchanganyiko na hakikisha uchanganya vizuri.
- Mimina kwenye sufuria au chombo cha kuchomea na huku unagandamiza gandamiza mchanganyiko kwa mkono hadi uwe umeshikamana.
- Kisha weka maridadi juu kwa kuchovya kwa uma.
- Choma kwenye oveni moto wa 350°F kwa muda wa saa 1 na robo hivi; Kisha iwache ipoe, kata vipande na itakuwa tayari kwa kuliwa na chai au kahawa
0 comments:
Post a Comment