Follow this blog with bloglovin

Ads

17-Tawhiyd Ndiyo Inayotenganisha Baina Ya Uislamu Na Ukafiri Au Baina Ya Muislamu Na Kafiri

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine (kuwa) waungu badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu (tunaojisalimisha kwa Allaah).” [Aal-‘Imraan: 64]

Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ ثَالِثُ ثَلَاثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿٧٣﴾

Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni watatu wa utatu.” Na hali hakuna ilaah (muabudiwa wa haki) isipokuwa Ilaah (Muabudiwa wa haki) Mmoja (Pekee). Na wasipoacha yale wanayoyasema, bila ya shaka itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu iumizayo. [Al-Maaidah: 73]


Neno la Tawhiyd “Laa ilaaha illa Allaah” ndio neno ambalo atakapolitamka mtu akiwa anakiri moyoni kwamba hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na kumalizia kuamini kwamba Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mja na Rasuli wa Allaah, humuingiza katika Uislamu. Lakini Uislamu wake utatimia kikamilifu pale atakapoamini  kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa Hana mshirika na atakapofuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake. Vilevile kumwamini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kuamini kwamba hakuna ‘ibaadah au mafunzo yoyote yale isipokuwa aliyokuja nayo yeye Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Muislamu  atakapothibitika nalo neno la Tawhiyd, huwa ni ufunguo wake wa Jannah.

عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :((مَنْ قَالَ: "أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللَّهِ وَابْنُ أَمَتِهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ وَأَنَّ الْجَنَّةَ حَقٌّ وَأَنَّ النَّارَ حَقٌّ" أَدْخَلَهُ اللَّهُ مِنْ أَيِّ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةِ شَاءَ))
Imepokelewa toka kwa ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit ambaye amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam): ((Atakayesema: “Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka lahu, wa anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu – Nashuhudia kwamba hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Peke Yake, Hana mshirika na kwamba Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah, na ni mwana wa mja wake na Neno Lake Alimtupia Maryam ana Ruwh kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na Moto ni haki” Allaah Atamuingiza Jannah kupitia mlango wowote autakao miongoni mwa milango minane ya Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Abu Twaalib ambaye ni ‘ammi yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataa kutamka neno la Tawhiyd wakati alipokuwa anafariki, na hivyo juu ya kuwa ni ‘ammi yake ambaye alimhami na maudhi ya makafiri Quraysh wa Makkah, amehukumiwa Moto.

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أَهْوَنُ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا أَبُو طَالِبٍ وَهُوَ مُنْتَعِلٌ بِنَعْلَيْنِ يَغْلِي مِنْهُمَا دِمَاغُهُ))‏

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wasallam) amesema: ((Adhabu nyepesi kabisa ya watu Motoni ni adhabu ya Abu Twaalib, atakuwa amevaa viatu [vya moto] vitakavyomsababisha bongo lake kuchemka)). [Muslim]


Na kisa cha kijana wa kiyahudi aliyesilimu:

فعَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ غُلَامٌ يَهُودِيٌّ يَخْدُمُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَمَرِضَ، فَأَتَاهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَعُودُهُ، فَقَعَدَ عِنْدَ رَأْسِهِ فَقَالَ لَهُ: أَسْلِمْ! فَنَظَرَ إِلَى أَبِيهِ وَهُوَ عِنْدَهُ، فَقَالَ لَهُ أَطِعْ أَبَا الْقَاسِمِ، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ . فَأَسْلَمَ ، فَخَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يَقُولُ : ((الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنْقَذَهُ مِنْ النَّارِ))
Imepokelewa toka kwa Anas (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba kulikuweko na mtoto (kijana mdogo) wa kiyahudi akimhudumia Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alipoumwa, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikwenda kumtembelea, akaketi pembeni ya kichwa chake akamwambia: ((Silimu!)). Mtoto akamtazama baba yake aliyekuweko hapo. Akamwambia: “Mtii Abal-Qaasim Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam”.  Akasilimu. Kisha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatoka huku akisema: ((AlhamduliLLaah – sifa njema ni za Allaah Ambaye amemuokoa na Moto)). [Al-Bukhaariy (1356), Ahmad (13565) na Abu Daawuwd (3095)]


Na Tawhiyd ndio sababu ya Al-Walaa wal-Baraa (Kupendana kwa ajili ya Allaah (Dini) na kuchukiana au kutengana kwa ajili ya Allaah)

Na ndio maana Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na usuhuba na mapenzi na Bilaal na Maswahaba wengineo waliokuwa watumwa ambao waliingia katika Uislamu kwa sababu ya Dini, na akatengana na Abu Twaalib na Abu Lahab kwa sababu ya Dini. Hali kadhaalika Maswahaba walitengana na baadhi ya ahli zao kwa sababu ya ukafiri wao. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):


لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚأُولَـٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚرَضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚأُولَـٰئِكَ حِزْبُ اللَّـهِ ۚ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّـهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ﴿٢٢﴾

 

Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho (kuwa) wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa (ni) baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao (Allaah) Amewaandikia katika nyoyo zao iymaan, na Akawatia nguvu kwa Roho kutoka Kwake, na Atawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito ni wenye kudumu humo. Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Hao ndio kundi la Allaah. Tanabahi! Hakika kundi la Allaah ndio lenye kufaulu. [Al-Mujaadalah: 22]

SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: