- Tunapaswaa kujua utukufu wa mwenyezi mungu mtukufu na uwezo wake na kwamba kakizunguka kila kitukwa elimu yake, maana utukufu wa viumbe ni dalili ya utukufu wa aliye viumba
- Kuwaamini malaika kunatuhamasisha katika kufanya yaliyo mema na kutengana na mabaya, kataka hali ya siri na uwazi,pindi pale muislamu anapotambua kuwa kuna malaika wanao sajili maneno yake na vitendo vyake, na kwamba kila alifanyalo litakuwa ima la kheri au la shari.
- Kuwaamini malaika kunatusaidia kutengana na mambo ya uzushi, na itikadi batili walizonazo wasio amini ghaibu(mambo yasiyo onekana).
- Tunapata kujua huruma ya mwenyezi mungu kwa waja wake, kwa kule kuwaekea malaika wanao wahifadhi na kuyaendesha mambo yao.
- Kuviamini vitabu,Ni kuamini mwenyezi mungu mtukufu, kateremsha vitabu kutoka kwake,kaviteremsha kwa mitume wake,ili wavifikishe kwa watu, na kwamba vitabu hivyo vimebeba haki, na kumpwekesha mwenyezi mungu katika uungu wake na uumbaji wake na katika majina na sifa zake. Amesema mwenyezi mungu mtukufu;"kwa hakika tuliwapeleka mitume mitume wetu kwa dalili za waziwazi na tukaviteremsha vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu"Al- hadyd;25, Na mwislamu anatakiwa kuviamini vitabu vyote vilivyo teremshwa kabla ya qur-ani, na kuamini kuwa vinatoka kwa mwenyezi mungu, lakini hawajibiki kuvifanyia kazi na kuvifuata bada ya kushuka qur-ani, kwa sababu vitabu hivyo vimeteremsha kwa muda maalumu na kwa watu maalumu. miongoni mwa vitabu hivyo ambavyo mwenyezi mungu kavielekeza ni:
- Swahifu za ibhrahimu na musa
- Taurati
- Zaburi
- Injili
- Qur-ani tukufu
imechapishwa na:
shafii bin omary
0 comments:
Post a Comment