Chai ya masala ni chai ya viungo (spices) ambayo unaweza kuipika vile unavyopenda, aidha ya maziwa au kavu, nikija upande wangu mimi napenda sana chai kavu, ila nikitamani chai ya maziwa lazima iwe ya masala ,
MAHITAJI
Maziwa ya maji lita 1
Majani ya chai pakti 2 au vijiko 2 vya supu
Zaatari kijiko 1 cha chai
Iliki chembe 3
Karafuu kavu chembe 3
Mdalasini kipande 1 cha kiasi
Tangawizi mbichi au kavu kiasi unachopenda
Sukari
Weka vitu vyote kwenye sufuria isipokua tangawizi na sukari , unaweza kuengeza na maji au ukawacha maziwa matupu,
Weka vitu vyote kwenye sufuria isipokua tangawizi na sukari , unaweza kuengeza na maji au ukawacha maziwa matupu,
Iweke kwenye moto wacha ichemke vizuri,
Ikichemka vizuri kama imefanya mapovu juu ikoroge yale mapovu yaondoke,
Hakikisha imeshachemka vizuri kwa dakika angalau 2 , saga tangawizi na utie kwenye chai, moto usiwe mdogo maziwa yanaweza kukatika , wacha ichemke tena kwa dakika 1 na epua , ichuje na Iweke/itie kwenye chupa au vikombe.
- Unaweza kuweka sukari kabisa au unaweza kukorogea kwenye kikombe
- Ili maziwa yasikatike hakikisha chai imechemka vizuri kabla kuweka tangawizi, AU yachemshe maziwa pekee kwanza mpaka yachemke vizuri ndio utie vitu viliobaki
- Sufuria ya kupikia chai isiwe unapikia vyakula vyengine , bila hivo inaweza kusababisha chai/maziwa yakatike
- Ukipenda unaweza kutia mchaichai na pilipili manga, inazidi kua tamu.
0 comments:
Post a Comment