Follow this blog with bloglovin

Ads

22-Tawhyd Ni Sharti Ya Kuingia Jannah

Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
((لاَيَدْخُلُ الْجَنَّةَ إِلا نَفْسٌ مُؤْمِنَةٌ))
((Hatoingia Jannah isipokuwa nafsi iliyoamini))

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ يُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ حِسَابٍ﴿٤٠﴾
na yeyote atakayetenda (‘amali) nzuri kati ya mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Jannah wataruzukiwa humo bila ya hesabu.  [Ghaafir: 40]

Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
((مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ وَالْجَنَّةُ حَقٌّ وَالنَّارُ حَقٌّ أَدْخَلَهُ اللَّهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنْ الْعَمَلِ))
((Atakayeshuhudia/atakayeamini moyoni na kukiri kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na neno Lake Alilompelekea Maryam na Ruwh kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na Moto ni haki, Allaah Atamuingiza Jannah kwa ‘amali zozote alizonazo)). [Al-Bukhaariy (3/1267) (3252), Muslim (1/57) (28) Ahmad (5/313) (22727), Ibn Hibbaan (1/431) (202), An-Nasaaiy (6/331) (11132)

Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisema:
((يَا أَبَا هُرَيْرَةَ (وَأَعْطَانِي نَعْلَيْهِ) قَالَ: اذْهَبْ بِنَعْلَيّ هَاتَينِ فَمَنْ لَقِيتَ مِنْ وَرَاء هَذَا الْحَائِطِ يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّهُ مُسْتَيْقِنا بِهَا قَلُبُهُ فَبَشّرْهُ بِالْجَنّةِ))
((Ee Abaa Hurayrah (akanipa viatu vyake) Nenda na viatu vyangu hivi, utakayemkuta nyuma ya ukuta huu akiwa anakiri moyoni na anashuhudia kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki ila Allaah akiwa amethibitika nayo moyoni, mbashirie Jannah)). [Muslim]
Hadiyth ya ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

((مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّة))
((Atakayefariki akiwa anajua kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah ataingia Jannah)). [Muslim]
SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: