Makafiri Quraysh wa Makkah walitaka kumpa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mali na starehe za dunia, walitaka kumpa cheo ili aache kulingania Tawhiyd lakini Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakufadhilisha hayo, bali alijikita katika da’wah yake kwa kuwa aliamini kulingania Tawhiyd ndio haki na ndio itakayomfaa bin Aadam Siku ya Qiyaamah, Siku ambayo mtu atatamani kufidia kwa mali yake yote aliyokuwa nayo duniani ili aepukane na adhabu ya Moto kwa kukanusha Tawhiyd. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾
Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi haitokubaliwa kutoka kwa mmoja wao (fidia ya) dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wakitaka kujikombolea nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata mwenye kuwanusuru. [Aal-‘Imraan: 91]
Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hadiyth iliyosimuliwa na Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu):
((يَقُولُ اللهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى لِأَهْوَنِ أَهْلِ النَّارِ عَذَابًا: لَوْ كَانَتْ لَكَ الدُّنْيَا وَمَا فِيهَا، أَكُنْتَ مُفْتَدِيًا بِهَا؟ فَيَقُولُ: نَعَمْ ، فَيَقُولُ: قَدْ أَرَدْتُ مِنْكَ أَهْوَنَ مِنْ هَذَا وَأَنْتَ فِي صُلْبِ آدَمَ: أَنْ لَا تُشْرِكَ - أَحْسِبُهُ قَالَ: وَلَا أُدْخِلَكَ النَّارَ - فَأَبَيْتَ إِلَّا الشِّرْك))
((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Atamwambia mtu atakayekuwa na adhabu nyepesi kabisa Motoni “Je, ungekuwa una dunia nzima na yaliyomo ndani yake [mali n.k.] ungeitolea fidia?”)) Atajibu ((Ndio)) Atasema Allaah: ((Nilikutaka kwa jambo jepesi zaidi kuliko hayo, ulipokuwa katika uti wa mgongo wa Aadam kwamba usinishirikishe)) Nadhani Akasema: (na sitokuingiza motoni lakini umekataa isipokuwa kunishirikisha)).[Muslim]
Ni dhahiri kwamba Tawhiyd ambalo ni jambo jepesi kabisa itakuwa na thamani zaidi kuliko dunia na yaliyomo duniani, bali neno la Tawhiyd; laa ilaa illa Allaah litakuwa zito kabisa katika Miyzaan ya ‘amali Siku ya Qiyaamah:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرَيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ الله (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((قَالَ مُوسَى عَلَيْهِ السَّلامُ يَا رَبِّ! عَلِّمْنِي شَيْئًا أَذْكُرُكَ وَأَدْعُوكَ بِهِ. قَالَ: قُلْ يَا مُوسَى: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ. قَالَ يَا رَبِّ! كُلُّ عِبَادِكَ يَقُولُونَ هَذَا. قَالَ: يَا مُوسَى, لَوْ أَنَّ السَّمَوَاتِ السَّبْعَ وَعَامِرَهُنَّ غَيْرِي وَالأَرَضِينَ السَّبْعَ فِي كِفَّةٍ, ولاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ فِي كِفَّةٍ، مَالَتْ بِهِنَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ)) رَوَاهُ ابْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ.
Imepokewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudhriyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muwsaa alisema: Ee Mola wangu! Nifundishe kitu ambacho kwacho nikudhukuru na nikuombe du’aa. Akasema [Allaah]: Ee Muwsaa:Sema: “Laa ilaaha illa-Allaah”. Muwsaa akasema: Ee Mola wangu! Kila mja anasema hivi. Akasema [Allaah]: Ee Muwsaa, lau kama mbingu saba na kila kilichokuwemo isipokuwa Mimi, na ardhi saba zikiwekwa katika kiganja cha mizani, na laa ilaaha illa-Allaah imewekwa katika kiganja kingine cha mizani, basi laa ilaaha illa-Allaah itazishinda hizo)). [Ibn Hibaan na Al-Haakim, na ameikiri kuwa ni Swahiyh].
0 comments:
Post a Comment