Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾
Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hakuna ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Mimi; basi Niabuduni.” [Al-Anbiyaa: 25]
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ
Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (awaamrishe watu wake) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaaghuwt (miungu ya uongo). [An-Nahl: 36]
وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ ﴿٤٥﴾
“Na waulize wale Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Rasuli Wetu; je, Tulifanya badala ya Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) miungu mingine iabudiwe?” [Az-Zukhruf: 45]
‘Allaamah Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema katika mhadhara wake: “At-Tawhiyd Yaa Ibaada Allaah”: “Mitume wote kuanzia wa mwanzo wao hadi wa mwisho wao, walianza kulingania kwao watu kwa Tawhiyd, kwa kuwa Tawhiyd ndio msingi ambao Dini imejengeka. Tawhiyd ikiwa imara, nyumba itasimama vizuri na kuwa imara. Na huu ni mfano wa misingi ya majumba na majengo; kwanza huanza kwa kujenga msingi ukawa imara kisha ndio kukajengwa nyumba na kupandishwa. Nyumba haiwezi kusimama bila ya msingi imara. Lau utajenga nyumba bila ya msingi imara wenye nguvu, basi nyumba itaporomoka na kuangamia waliomo humo ndani. Hali kadhalika Dini ikiwa haikujengeka katika ́Aqiydah swahiyh, inakuwa ni dini isiyomfaa mtu na wala haimnufaishi chochote, hata kama atajitaabisha vipi kufanya juhudi. Dini yake haitomfaa kitu, kwa kuwa haikujengeka juu ya msingi swahiyh, nao ni Tawhiyd. Kwa ajili hio, kitu cha kwanza walichoanza Rusuli (‘Alayhimus-Salaam) kuwalingania watu wao, ilikuwa ni Tawhiyd, nayo ni kabla ya kuwaamrisha Swalaah, Zakaah, Swawm n.k. Na ilikuwa ni kabla ya kuwakataza zinaa, wizi, kunywa pombe na maasi mengine, walianza kwanza kwa msingi ambao ni Tawhiyd. Na kila Nabiy alimwambia kaumu yake:
يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ
Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah (Pekee); hamna ilaah (muabudiwa wa haki) ghairi Yake.”
[Mwisho wa kunukuu maneno ya ‘Allaamah Al-Fawzaan].
Dalili hizo zimo katika Qur-aan:
Nabiy Nuwh (‘Alayhis-Salaam):
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٢٣﴾
Kwa yakini Tulimpeleka Nuwh kwa kaumu yake, akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah (Pekee); hamna ilaah (muabudiwa wa haki) ghairi Yake. Je, basi hamuwi na taqwa?” [Al-Muuminuwn: 23]
Nabiy Huwd (‘Alayhis-Salaam):
وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴿٦٥﴾
Na kwa ‘Aad (Tuliwapelekea) kaka yao Huwd. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah (Pekee), hamna ilaah (muabudiwa wa haki) badala Yake. Je, hamuwi na taqwa?” [Al-A’raaf: 65]
Nabiy Swaalih ('Alayhis-Salaam):
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ
Na kwa Thamuwd (Tuliwapelekea) kaka yao Swaalih. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah (Pekee), hamna ilaah (muabudiwa wa haki) ghairi Yake. [Al-A’raaf: 73]
Nabiy Shu’ayb ('Alayhis-Salaam):
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ
Na kwa (watu wa mji wa) Madyan (Tuliwapelekea) kaka yao Shu’ayb. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mwabuduni Allaah (Pekee) hamna ilaah (muabudiwa wa haki) ghairi Yake” [Al-A’raaf: 85]
Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam):
وَإِبْرَاهِيمَ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاتَّقُوهُ ۖ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿١٦﴾
Na (kumbusha pale) Ibraahiym alipowaambia kaumu yake: “Mwabuduni Allaah na mcheni. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua. [Al-‘Ankabuwt: 16]
Nabiy Muwsaa ('Alayhis-Salaam):
وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِاتِّخَاذِكُمُ الْعِجْلَ فَتُوبُوا إِلَىٰ بَارِئِكُمْ
Na (kumbukeni wakati) Muwsaa alipowaambia kaumu yake: “Enyi kaumu yangu! Hakika nyinyi mmedhulumu nafsi zenu kwa kumchukua kwenu ndama, basi tubuni kwa Baariu (Muumbaji) wenu. [Al-Baqarah: 54]
Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam):
لَقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ الْمَسِيحُ يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اعْبُدُوا اللَّـهَ رَبِّي وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿٧٢﴾
Kwa yakini wamekufuru wale waliosema: “Hakika Allaah ni Al-Masiyh mwana wa Maryam.” Na Al-Masiyh alisema: “Enyi wana wa Israaiyl! Mwabuduni Allaah, Rabb (Mola) wangu na Rabb wenu. (Kwani) Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni Motoni. Na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.” [Al-Maaidah: 72]
Na Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye aliwalingalia watu wake waliokuwa wakiabudu masanamu, miaka kumi na tatu alipokuwa Makkah kwa Tawhiyd kabla ya kufaridhishwa Swalaah, Zakaah, Swawm au Hajj.
عن ابنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أنَّ رسُوَل الله صلى الله عليه وسلم قال: ((أُمِرْتُ أَنْ أُقاتِلَ النَّاسَ حتَّى يَشْهَدُوا أنْ لا إلَهَ إلاَّ اللهُ وأنَّ محمداً رسوُل اللهِ، ويُقِيمُوا الصَّلاَةَ، ويُؤتُوا الزَّكاةَ، فإذا فَعَلوا ذَلِكَ عَصَموا منِّي دِماءَهُمْ وأمْوَالَهُمْ إلا بِحَقِّ الإِسْلامِ، وحِسابُهُم على اللهِ تعالى)
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Umar (Radhwiyaa Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nimeamrishwa nipigane na watu mpaka washahadie kuwa hakuna ilaah (muabudiwa wa haki) isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah mpaka watakaposwali, na wakatoa Zakaah na wakifanya hivyo, watakuwa wamepata himaya kwangu ya damu yao na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislamu. Na hesabu yao itakuwa kwa Allaah Ta’aala)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
0 comments:
Post a Comment